Alhamisi 25 Septemba 2025 - 07:26
Msaada kwa Palestina kamwe hauwezi kuyumba

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hasan Mousavi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Kishia Jammu na Kashmir, katika hotuba yake alikataa kwa dhati mpango wa dola mbili na kutaka kuundwa kwa dola moja ya kidemokrasia nchini Palestina, alisisitiza kuwa msaada wa mataifa yanayoyapenda haki duniani kwa haki za Wapalestina hauterereki kamwe.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Hasan Mousavi alisema kwamba mataifa yanayoyapenda haki duniani yatakuwa kando ya malengo ya Palestina kwa hali yeyote ile, hakuna sababu au hali yoyote inayoweza kudhoofisha kuwasaidia watu wanyonge duniani kama Palestina; msaada huu una mizizi yake katika dhamira iliyokuwa hai ya kibinadamu.

Alipokuwa akikosoa baadhi ya nchi zinazounga mkono mpango wa dola mbili, alisisitiza kuwa mtazamo huo hauendani na ukweli na kupitia njia hiyo, taifa la Palestina halitawahi kupata haki zake halisi.

Hujjatul-Islam Sayyid Hasan aliongeza kuwa; jumuiya yake inaunga mkono tu kuundwa kwa dola moja ya kidemokrasia nchini Palestina, ambayo itahusisha wananchi wote wa asili wa Palestina, iwe wakazi wa ardhi zilizo chini ya uvamizi au wakimbizi walioko nje ya nchi, alisisitiza kuwa wazo la kuunda dola mbili haliwezi kukubaliwa kwa namna yoyote.

Akizungumzia hali mbaya ya Ghaza, alisema: “Wananchi masikini wa Ghaza wanakabiliwa na maumivu yasiyoelezeka yanayotokana na vita vya kimbari vya Waisraeli, hadi sasa, idadi ya mashahidi imezidi 60,000, wengi wao ni wanawake na watoto wasio na hatia.”

Alieleza kuwa mgogoro wa Palestina, hususan Ghaza, ni wa kuonyesha hofu kubwa, hali hii si tu maafa ya kibinadamu, bali ni dhulma kubwa ya kihistoria dhidi ya taifa lililokosa haki za msingi za kibinadamu na heshima ya asili kwa zaidi ya vizazi saba, na kuwa kando ya uvamizi na ukatili.

Sayyid Hasan Mousavi pia alikosoa kwa ukali siasa za Magharibi, akisema kuwa nguvu za Magharibi mara nyingine tena hazikuzingatia mizizi ya mgogoro na badala ya kutii misingi ya haki na haki za binadamu, waliweka urafiki wao wa kimkakati na utawala wa Kizayuni juu ya kila kitu.

Mwisho, alikumbusha kuwa utawala wa Israeli, ukiwa unategemea msaada usio na masharti kutoka baadhi ya nguvu, unafanya vitendo vinavyowakilisha wazi jinai kubwa za kimataifa, ikiwemo uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya binadamu, ubaguzi wa kikabila, ubaguzi wa rangi na mauaji ya halaiki.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha